Niaje WaKenya...na pia wale si waKenya,mko vepeee!!. Waaaah!!
Io ni mimi nikipumua juu yenyewe niliwaga nimefungia mafikra mia kadhaa hadi saa izi. Lakini acha tucheki Morgan Anan ama ni Koffi Freeman...kaa ataeza kutandika io bandage vifiti mathaland iache ku-bleed.
Ii valentino(yani si I'd written this kitambo, thanks for noting) sijui RED ilikuwa colour ya ma-lové ama ni ile damu iliwaga imemwagika, kitu najua upendo iko. Kaa venye mi nawapenda.....nyo..nyote
Nakumbuka ii noma saa zenye ilianza ilibidi nimekwenda kusukuma mawiki na kuzo yangu uko Umo. Saa kitu ilinishaga na io time ni venye tuliwaga tunasota kishenzi. Alafu unajua tubidhaa bidhaa tuliwaga tumepandanga bei. Ati airtime ya chwani 70/- Maziwa 50...fyanje!!...na bei zingine apo funni funni. Saa si mambo zilizuka kitu Sunday ivi...io Wednesday asubuhi ivi, tuliwaga tumebakisha ka40 bob pekee. Kuzo hufwaka. Iliwagga imefika point ingine dezine hangengoja, kiu ilikuwa imetach baze wazimu. Saa juu iliwaga ile coin ya 40 bob na ni mi niliwaga nayo, jamaa akanikamia kuniskizisha ati nimkanje akanunue “bre?-breko” (Heheh!!)...tu-mahamri ivi ivi. Mi niliwaga najua ujanja yake kwa ivo nikamwambia nitaenda kununua mi mwenyewe. Jamaa kuona hatoboi kuni-convince ni mpatie ile 40, akaamua ataniwai push hadi kwa duka....Man! Si tulikutanga maduka karibu zote around io area zimetingwa, zingine zimefanyiwa 'ukarabati'. Lakini matha mwenye aliwaga akipika tule tumahamri...aliwaga amefungua. Kwenda kununua mahamri anatwambia sijui ati 12 bob, samthing tulikuwa tuki-buy ngovo...Asi! Saa mi nafanya thafu kwa kichwa venye tutamanga breko na nifike mtaani kuangalia kaa naeza sakanya ka-mkwanja mdogo ata kaa ni ya siku mbili...Napata maDeficit tu...kuzo akauliza yule mthama kaa aliwaga amebakisha fwaka/fegi. Saa mi nikamwangalia nashindwa nimwabie nini...Mathe akamwambia ziko. Kuskia ivo..
Kuzo(K): Aaah We! Mi ninunulie Safari tatu na Big G...staki ma-amri...
Mimi: Kwani leo unavuta Safari?
Aliwaga akivuta SuperMatch.
K: Kaa utanunua Emba sina tabu.
Mimi: We kwanza acha nifikirie...
K: Unafikiria nini?! Si ni ndeki(10) tu!!
Mimi: We unajua bado nafika mtaani leo?
K: We du ivi, mpatie io kinde, Tutafikiria risto yako badae...
Mimi: Tutafikiria nini mdosi, we unajua nina 40-bob!!
K: Mama Mtunga Safari unauza ngapi?
Mathe: Tatu shilingi nne...
Mimi:Aki ya nani na venye nina njaa! Mathe si utupatie ma-amri tutakulipa leo jioni...
Mathe akatingisha kichwa...
K: Wee Kaa unanjaa utapika sembe kejani...ninunulie feggi bana!!
Saa ii huskii nikatoa ile 40 bob nikaambia yule mathe anipatie mahamri mbili...(Za uyu Mathe, ukidishi mbili nikaa nne za kawaida). Ukweli ni; kuzo huwaga hapiki, io unga ya sembe ni mi niliwaga nimeletanga...na iliwaga karibu kuisha.
K: Na uongeze feggi mbili basi...
Yule matha kumbe aliwaga na dezine zake ulterior kwa interior yake...Akachukua ile 40 bob...alafu afta kuiweka akaniambia ati Domi(Kuzo) aliwaga na deni yake ya feggi ya 30 bob. Matha akapatia Domi Safari mbili...Saa ii mi nimeshtuka ata sikuleta tafash...Domi kimechapanga kiSmilo stupid tu...Mama Mtunga akanirudishia 7 bob...Nikamwambia anipatie ma-gum io shilingi saba...Io day nilikulanga ma-gum breko. Alafu mabadae nikachapanga guu ingine Olympic class...toka Umo hadi mtaani (Hukoooo...Hehehe!!), through Buru, Jerri na Marish.
Mafikra, ngumu kama kupokonywa ubikra-Sewer
Wacha ata mimi ni niseme venye nimechukianga awa wanasaisa, WOTE!! Wote ni maNgamia bila mikia. Ata io ni sifa..Aki ya nani awa mafisi hawataki kuacha kutunyad pande zote...Ata saa ii wanazidi kuleta sheshe kwa izi ma-talks za Anan badala ya kufikiria venye watapata majibu, na ma-resolution ili wathii watulie angalua mdogo...ma-arrow ziache ku-fly, Ma-freesk waache ma-massacre na umati itulie in general. Niliskianga msomi flani akisema ati ii ni vita ya social Justice...mi nilionanga iyo ikiwa ukweli kiPlani...Lakini mi si msomi kwa ivo sitabonga juu ya mafikra za wengine.
I once watched this Indian movie...how fast can you say “Bolly is Big”, thing about it was there was an offal (<<--Io spelling maze!!) lot of razor blades in that movie...one scene; a guy's (protagonist I think, me memory needs an upgrade) jaw is forcefully held open by this sweaty guy...I remember because he(the sweaty one) kept losing his grip on our guy's chin...aniwei the Otero (Bad Guy) skillfully goes ahead to slit the corners of his (the one held) mouth with the Nasset blade he has in his hand. Now the sweaty bugger loses his grip again and our guy, understandably feeling like the trio in the fiery furnace, jerks his head again from the agony and the blade slices further into his cheek.....Rrrrrrya!!!! Ama its Shweee!...Ok. I think the ideal sound is Shwaaa!! I'm not sure whats more unsettling...that the blade was Nasset or ammm that the guy's smile had been enlarged somewhat, in the crudest of ways. I just hate Razor blades from that time...especially the Nasset kind(red).
So...aah..shaving cream...Hihihihhihi!!! Ok. I can't go on...I'm laughing too hard...Ati shaving cream...Modo ukiongea wewe!! Hihihihih!!!
Ombea Kenya...scratch that Ombea Wakenya..
Inaonekana wewe ni mutu ya gufu kama umemalisa kusoma hii...